Home Azam FC AZAM WATAJA SABABU ZA KUPOKEA KICHAPO MBELE YA COASTAL UNION

AZAM WATAJA SABABU ZA KUPOKEA KICHAPO MBELE YA COASTAL UNION


UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa haukuwa na chaguo la kufanya Uwanja wa Mkwakwani jana kwa kuwa uwanja haukuruhusu wacheze mipira ya chini jambo ambalo liliwafanya wapoteze pointi tatu.


Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina ilikubali kuacha pointi tatu zote baada ya kufungwa mabao 2-1.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa aliongea na mwalimu na kumuuliza tatizo lipo wapi mwalimu aliweka wazi kwamba uwanja ulikuwa tatizo kwao kuwa haukuruhusu mipira ya chini.

“Haukuwa uwanja rafiki kwetu kwa kuwa ulikuwa hauruhusu mipira ya chini jambo ambalo limetufanya tushindwe kupata matokeo chanya ndani ya uwanja.

“Ukiangalia kwa takwimu vijana wetu walipambana na kufanya vizuri ila wapinzani wetu waliweza kupiga mashuti mawili yaliyolenga lango na wakashinda hivyo tunajipanga kwa ajili ya mechi zijazo,”.
 
SOMA NA HII  AZAM FC KUTISHIA USALAMA WA LIGI KUU...VYUMA HIVI MATATA KUSAJILIWA