Home Habari za michezo ENG. HERSI: YANGA TUKO TAYARI KUMWACHA FEI TOTO AENDE…VYUMA VINAKUJA ZAIDI…

ENG. HERSI: YANGA TUKO TAYARI KUMWACHA FEI TOTO AENDE…VYUMA VINAKUJA ZAIDI…

Habari za Yanga

Klabu ya Yanga imesema wapo tayari kumwachia kiuongo wao mshambulizaji, Feisal Salum ‘Fei Toto’ kwenda nje ya nchi ambayo itafikia makubaliano na si kwa klabu yoyote ya ndani ya nchi kama ambavyo imekuwa ikisemwa.

Hayo yamesemwa na Rais wa Yanga, Eng. Hersi Said ikiwa ni siku chache baada ya tetesi kuanza kusambaa kuwa mchezaji huyo anataka kusajiliwa na matajiri wa Dar, Azam FC.

Aidha, Hersi amesema katika dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa wiki chache zijazo, Yanga itasajili wachezaji wa daraja la juu ili kuimarisha kikosi chao kuelekea mashindano ya kimataifa huku akisisitiza kuwa watawatangaza wachezaji wao alfajiri na kwamba wapo watakaoachwa na klabu hiyo.

“Niwahakikishie mashabiki na wanachama wote wa Yanga kwa sasa hakuna mchezaji ambaye anaweza kuondoka Yanga ambaye yupo kwenye mipango ya kocha mkuu Nabi.

“Sisi kama viongozi tumejipanga vyema kuhakikisha kila mchezaji wetu anafurahia kuwepo Yanga na kujua thamani ya logo na jezi ya Yanga.

“Tumetoka mbali sana na kuweka standard sawa kwenye kikosi siyo kazi ndogo leo hii kwenye timu yetu kila nafasi ina wachezaji wa daraja la juu kabisa sisi Kama viongozi tumepambana na hivyo hatutakubali kuona mchezaji wetu Kama Feisal salumu anaondoka kirahisi tu.

“Tupo tayari kumwachia kiungo wetu Feisal salumu kwenda nje ya nchi kama kuna timu itafikia makubaliano na sisi Yanga ila hatupo tayari kumwachia Feisal salumu kujiunga na timu yoyote hapa nchini ikiwemo Azam fc kwa gharama yoyote. Feisal salumu bado ni mchezaji wetu na ana mkataba na Yanga.

“Tumejipanga vyema kufanya usajili mzuri dirisha dogo hili kujazia tu baadhi ya nafasi ambazo kocha Nabi ametuambia ila kabla ya kuanza usajili mpya dirisha dogo Kuna baadhi ya wachezaji tutakwenda kumalizana nao kwa kuwaongeza mikataba mipya hivi karibuni tupo Katika mazungumzo nao kwa sasa na kila kitu kinakwenda sawa.

“Huu ndio muda sasa wa kuona baadhi ya timu zinataka kupata umaarufu kupitia Yanga sc kwa kusema Kuna mchezaji tumewashinda ila niwahakikishie tu usajili huu mdogo tunaleta top expensive players.

“Na Style yetu ni ilele tu ya kuwatambulisha wachezaji wetu wapya ila Kuna mmoja safari hii tutantangaza alfajiri kabisa.

“Kwa sasa nachowaomba mashabiki wetu na wanachama wetu kuendelea kutupa sapoti kwa kuendelea kujisajili kwenye mfumo mpya wa wanachama na mashabiki.

“Mambo mazuri yakuja kutoka kwa Viongozi wao tupo imara sana Yanga Sc. Niwaombe mashabiki wote Kutoka Singida na baadhi ya mikoa jirani kujitokeza kwa wingi siku ya Jumanne uwanjani Liti kwenye mchezo wetu dhidi ya Dodoma Fc,” amesema Hersi.

SOMA NA HII  BAADA YA AZIZ KI KUSHINDWA KUONYESHA KIWANGO JUZI....LUNYAMILA AIBUKA NA KUMNYOOSHEA KIDOLE...