Home Habari za michezo ROBERTINHO APIGA HESABU SIKU HIZI HAPA 16

ROBERTINHO APIGA HESABU SIKU HIZI HAPA 16

Habari za Simba leo

Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amefichua kwamba, amepanga kuzitumia siku 16 za mapumziko ya Ligi Kuu Bara kukijenga upya kikosi chake ili kuendana na kasi ya ligi msimu huu.

Robertinho ametoa kauli hiyo, Simba ikiwa inaongoza ligi ikiwa na pointi sita baada ya kucheza michezo miwili na kufunga mabao sita, huku ikiruhusu mawili.

Akizungumza Robertinho alisema kwa kuwa wanaenda kwenye mapumziko mafupi ya Ligi Kuu Bara kwa ajili ya kupisha michezo ya timu za Taifa, amepanga kutumia mapumziko hayo kukijenga upya kikosi chake ili kuendana na ushindani uliopo.

“Nimetoa mapumziko kwa wachezaji ambayo yatachukua siku nne, kisha siku 16 zitatumika kuhakikisha tunaendelea kujenga timu imara ambayo inaweza kuleta ushindani wakati wote, kwa sababu ukiangalia namna ligi ilivyoanza, unaona ni wazi kila timu ilivyojipanga kupata matokeo mazuri.

“Nadhani maboresho ya muda huo yatasaidia kuwa na timu ambayo italeta ushindani wakati wote, ukiangalia wapo wachezaji ambao walichelewa kufika wakati wa kambi, naamini kwa muda ambao tutaupata kila kitu kitakuwa kwenye ubora ambao tunaufikiria, ” alisema Robertinho.

SOMA NA HII  BAADA YA KUTUNGULIWA KIMOJA DAR...WYDAD WAAMUA KUFANYA MAAMUZI HAYA MAZITO...