Home Habari za michezo JKT SIO KINYONGE MBELE YA YANGA JAPO USHINDANI NI MKALI

JKT SIO KINYONGE MBELE YA YANGA JAPO USHINDANI NI MKALI

JKT TANZANIA WAENDELEZA UONEVU

Kikosi cha JKT Tanzania kinaendelea na mazoezi kujiwinda na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Yanga utakaopigwa keshokutwa, huku kocha mkuu wa timu hiyo, Malale Hamsini akiweka bayana ameandaa programu maalumu ya kuwafuatilia wapinzani wake.

JKT imerejea Ligi Kuu msimu huu kutoka Championship sambamba na Mashujaa na Kitayosce, na ilianza kwa ushindi wa bao 1-0 ikiwa ugenini Lindi dhidi ya Namungo na keshokutwa Jumanne itakutana na Yanga kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Malale alisema baada ya kuanza vyema ligi msimu huu anataka kuwa na mwendelezo kwa wachezaji, licha ya kukiri anakwenda kukutana na ushindani mkali.

SOMA NA HII  IBENGE AKOLEZA MOTO SAKATA LA CHAMA KURUDI TZ..AFUNGUKA SABABU ZA KUMPIGA BENCHI...