Home news IBENGE AKOLEZA MOTO SAKATA LA CHAMA KURUDI TZ..AFUNGUKA SABABU ZA KUMPIGA BENCHI…

IBENGE AKOLEZA MOTO SAKATA LA CHAMA KURUDI TZ..AFUNGUKA SABABU ZA KUMPIGA BENCHI…


KOCHA Mkuu wa RS Berkane ya nchini Morocco, Florent Ibenge, amefunguka suala la kiungo mshambuliaji wa zamani wa Simba, Clatous Chama, kushindwa kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara ndani ya kikosi hicho huku akiweka wazi kuwa mchezaji huyo anahitaji muda zaidi wa kukaa sawa ndani ya timu hiyo.

Chama alijiunga na RS Berkane mwanzo wa msimu huu akitokea Simba sambamba na winga wa zamani wa Yanga, Tuisila Kisinda.

Akizungumza hivi karibuni, Ibenge alisema kuwa suala la Chama kutokupata nafasi ya kucheza mara kwa mara ndani ya timu hiyo inatokana na mchezaji huyo kushindwa kuendana haraka na mazingira ya timu jambo ambalo linahitaji muda kidogo kwa mchezaji huyo kukaa sawa.

“Chama kushindwa kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara inatokea kwa wachezaji wengi wakubwa duniani ambao baada ya kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine wanashindwa kuendana na mazingira ya timu haraka jambo ambalo baadaye hubadilika baada ya kuyazoea mazingira, ni kama tu ilivyotokea kwa Chama.

“Hivyo Chama anahitaji muda wa kuyazoea mazingira ya timu ambayo ni mpya kwake, naamini atakuja kukaa sawa, Chama ni mchezaji mzuri mwenye uwezo mkubwa wa kucheza timu yoyote barani Afrika, hivyo ndio maana hata sisi tulimsajili, naamini kila kitu kitakuwa sawa huko mbeleni, ni jambo la muda tu,” alisema kocha huyo.

Hivi karibni kumeibuka tetesi kuwa Kiungo huyo kutoka Zambia anampango wa kutaka kurudi Tanzania kutokana na kushindwa kuendana na  mazingira ya soka la Morocco, huku akihusihwa zaidi kutaka kurudi Simba SC kwa mkopo.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA CAF KESHO KUTWA...MWAMNYETO AIWEKA YANGA KWENYE 'ENGO' NGUMU...