Home Habari za michezo HUYU MAKI HUYU….LEO KAIBUKA NA HILI LINGINE KUHUSU JOHN BOCCO…AENDELEA KUMTAJA ‘STRAIKA...

HUYU MAKI HUYU….LEO KAIBUKA NA HILI LINGINE KUHUSU JOHN BOCCO…AENDELEA KUMTAJA ‘STRAIKA MZUNGU’ WAKE….


Kocha Mkuu wa Simba SC Zoran Manojlović ‘Maki’ amevunja ukimya na kueleza sababu za kushindwa kumtumia Nahodha na Mshambuliaji wa kikosi chake John Raphael Bocco, kwenye Michezo miwili ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2022/23.

Simba SC ilichomoza na ushindi wa 3-0 dhidi ya Geita Gold FC Jumatano (Agosti 17), Kisha itakakutana na Kegera Sugar Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumapili (Agosti 21) na kuondoka na ushindi wa 2-0, huku Bocco akiachwa nje ya kikosi.

Kocha Maki amesema kukosekana kwa Mshambuliaji huyo mzawa, kulitokana na kukosa utimamu wa mwili, hivyo aliamua kumpa mazoezi maalum ili kurejea katika hali yake ya kawaida.

Hata hivyo kocha huyo kutoka nchini Serbia amesema Bocco atacheza michezo miwili ya Kimataifa ya Kirafiki nchini Sudan dhidi ya Asante Kotoko (Ghana) na Al Hilal (Sudan), ili kuangalia maendeleo yake, na baadae huenda akaanza kumtumia katika Ligi Kuu na Michuano ya Kimataifa.

“Bocco atacheza michezo miwili dhidi ya Asante Kotoko na Al Hilal kwa ajili ya kumuongezea utimamu wale wa mwili, naamini michezo hiyo itamsaidia kurudi katika hali yake iliyozoeleka.”

“Bocco alikua akifanya mazoezi vizuri, na hilo ni jambo zuri kwa timu kuwepo na mchezaji wa aina yake akiwa Fit. Uwepo wake kikosini unanipa machaguo mapana ya nafasi anayocheza, kwani kwa sasa watakuwepo Washambuliaji wanne pamoja na Dejan, Moses Phiri ambaye anaweza kucheza nafasi nyingine na Habibu Kyombo.”

“Dejan amefunga katika mchezo uliopita hali ya morari upande wake ipo juu kuendelea kutamani kufanya hivyo katika michezo inayofuata, na michezo hii ya kirafiki ataendelea kujengeka na kuzoea mazingira ya timu.” amesema Kocha Zoran Maki

Simba SC imeondoka jijini DAr es salaam mapema leo Alfajiri kuelekea Omdurman-Sudan kushiriki Michuano maalum iliyoandaliwa na Klabu ya Al Hilal ya nchi hiyo.

Simba SC itacheza dhidi ya Asante Kotoko keshokutwa Jumapili (Agosti 28) na Jumatano (Agosti 31) itapapatuana na wenyeji Al Hilal kwenye Uwanja wa Al Hilal mjini Amdurman-Sudan.

SOMA NA HII  MAMBO YAZIDI KUWA MAGUMU KWA CHAMA NA SIMBA...

Baada ya kurejea jijini Dar es salaam Simba SC itacheza mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya AS Arta Solar ya Djibout iliyoweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya jijini humo.