Home Burudani KUELEKEA PAMBANO LAKE NA ‘MZUNGU’….MWAKINYO APEWA ONYO…MSIRI WAKE WAKARIBU AFUNGUKA MENGI MAPYA…

KUELEKEA PAMBANO LAKE NA ‘MZUNGU’….MWAKINYO APEWA ONYO…MSIRI WAKE WAKARIBU AFUNGUKA MENGI MAPYA…


Aliyekua msaidizi wa Bondia Hassan Mwakinyo wakati akipambana kwa mara ya kwanza nchini England dhidi ya Sam Eggington, Nassoro Rashid ‘Chid’ amempa nafasi kubwa ya ushindi Bondia huyo kutoka Makorora jijini Tanga.

Mwakinyo atapanda ulingoni Septemba 03 jijini Liverpool kumkabili Bondia Liam Mark Smith, katika pambano la kuwania Ubingwa wa WBO.

Chid amesema anamfahamu vizuri Mwakinyo na anajua namna anavyojiandaa anapopata nafasi ya kupanda ulingoni Kimataifa, hivyo hana shaka na Bondia huyo ambaye ataikwakilisha Tanzania.

“Huyu Smith ni Bondia mkubwa ambaye ameshapigana na Mabondia wa viwango tofauti lakini atapigwa kama Mwakinyo akisimama na kuonyesha uhodari wake, ninafahamu ana uwezo mkubwa na ana utulivu, hivyo hatuna wasiwasi.”

“Ninachomuomba Mwakinyo ajiandae vizuri na awe mtulivu, kwa sababu anafahamu anakwenda kupambana na Bondia wa aina gani, ninarudia tena sina wasiwasi kabisa kwa sababu Mtanzania mwenzetu anajua namna ya kukabiliana na watu kama hawa.” amesema Chid

Amesema hata alipokua akimsaidia wakati wa pambano wa Eggington mwaka 2018 hawakufanyiwa Figisu zozote, hivyo kama Mwakinyo atapita kwenye njia zile zile, basi Septmba 03 mambo yatakuamazuri kwake.

“Kwa Smith akatafute matokeo ya TKO au KO la sivyo ahakikishe anaongoza Raund zote (Kuanzia mwanzo hadi mwisho). akifanya hivyo ushidi ni wake maana England hakuna Figisu Figisu kwa Bondia mgeni.

Mwakinyo mwenye nyota tatu na nusu atambana na Liam Smith mwenye nyota nne ambaye ni mzoefu akiwa amecheza Mapambano mengi 35, na kati ya hayo ameshinda Mapambano 31, akipoteza matatu na kupata sare katika Pambano moja.

Kwa upande wa Mwakinyo amecheza Mapambano 22, kati ya hayo ameshinda Mapambano 20 na kupoteza mawili. Kati ya 20 aliyoshinda, 14 ameshinda kwa KO na TKO.

Iwapo Mwakinyo atashinda Septamba 03, atazidi kupanda katika viwango vya Ubora Kimataifa, na itakua ni mara ya pili anapigana na Bondia kutoka England, baada ya mwaka 2018 kumpiga Sam Eggington katika Pambano lililounguma mjini Birmingham.

SOMA NA HII  MANARA:- "SIMBA WAKIPATA HATA SARE...WACHINJE NGAMIA SABA...ATEMA CHECHE HIZI