Home Habari za michezo BAADA YA KULA PESA ZA KUTOSHA BONGO TENA KIULAINI KABISA….MOLINGA AAMUA KUKIMBILIA...

BAADA YA KULA PESA ZA KUTOSHA BONGO TENA KIULAINI KABISA….MOLINGA AAMUA KUKIMBILIA ALIPOTOKA…


Mshambualiji wa zamani wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans David Milinga ‘Falcao’, huenda akajiunga na Zanaco FC ya Zambia katika kipindi hiki cha usajili wa 2022/23.

Molinga anatajwa kuwa kwenye mpango huo, baada ya kuachana na Namungo FC inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya pande hizo mbili kushindwa kufikia makubaliano ya kusaini mkataba mpya.

Uongozi wa Zanaco FC umeripotiwa kuwa katika mazungmzo na Mshambuliaji huyo, baada ya kupendekezwa na Kocha Mkuu Kelvin Kaindu anayedaiwa kuwa na mawasilino ya karibu na Kocha Mkuu wa Namungo FC Hanour Janza.

Inaelezwa kuwa wawili hao walianza mazungumzo baada ya kikosi cha Zanaco FC kufanya ziara nchini m mapema mwezi huu na kucheza mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki dhidi ya Singida Big Stars, mjini Singida.

Kama dili hilo litakamilika, hii itakua mara ya pili kwa Mshambuliaji huyo kucheza Ligi Kuu ya Zambia akitokea Tanzania, awali alisajiliwa na ZESCO United siku chache baada ya kuachana na Young Africans.

SOMA NA HII  WAKATI YANGA WAKIJIUMAUMA KWA NABI....SIMBA WAPANGA KUIFANYIA 'JAMBO BAYA' AZAM FC..