Home kimataifa LUKAKU ACHEKELEA KURUDI CHELSEA

LUKAKU ACHEKELEA KURUDI CHELSEA


 MSHAMBULIAJI Romelu Lukaku raia wa Ubelgiji amesema kuwa anafuraha ya kurudi ndani ya kikosi cha Chelsea ambapo atakuwa hapo kwa msimu ujao ndani ya Ligi Kuu England.

 Lukaku amerejea ndani ya Chelsea baada ya kuyeyusha miaka 10 kwa kuwa alisepa hapo mwaka 2014 na dau lake la usajili ni pauni milioni 97.5 akitokea Inter Milan.

Amesaini dili la miaka mitano kwa ajili ya kuwa ndani ya Stamford Bridge huku akiweka wazi kwamba anafuraha ya kurejea hapo.

“Ninafuraha kurudi hapa, nilikuwa ninaisapoti Chelsea tangu nikiwa mdogo na sasa nimerejea ninafurahi sana,” .

SOMA NA HII  ALABA AKUBALI KUTUA REAL MADRID