Home Habari za michezo SAA CHACHE KABLA YA KUKUTANA NA YANGA KESHO….WASUDAN WAENDELEA KUWEWESEKA NA MAYELE…FEI...

SAA CHACHE KABLA YA KUKUTANA NA YANGA KESHO….WASUDAN WAENDELEA KUWEWESEKA NA MAYELE…FEI TOTO KUTIWA PINGU…


Kocha Mkuu wa Zalan, Mawein Deng amewataja Fiston Mayele na Feisal Salam ‘Feitoto’ kuwa ndio wachezaji anaowahofia zaidi hapo kesho.

Wawili hao ndio walio wafunga kwenye ushindi wa mabao 4-0 huku Mayele akiingia kambani mara 3 na Fei Toto akifunga bao moja.

Akizungumzia mchezo kwa ujumla alisema timu yake imefanyia kazi makosa waliyoyafanya kwenye mchezo uliopita wamejiandaa vizuri kwa mchezo wa kesho.

“Tunatarajia mchezo mzuri na wa ushindani tumejiandaa kushindana lolote linaweza kutokea Yanga ni timu kubwa inawachezaji wengi wazuri lakini tunahofia zaidi mchezaji aliyevaa jezi namba 9 (Mayele) na namba 6 (Fei Toto),” alisema na kuongeza.

“Tumekuja kupambana tutapambana hadi dakika ya mwisho bado tuna nafasi ya kufanya kitu  dakika 90 ndio zitaamua nani anatakiwa kuendelea hatua inayofuata,”

SOMA NA HII  YANGA NA SIMBA... ZIMETUHAKIKISHIA KUPELEKA TIMU 4 KIMATAIFA MSIMU UJAO