Home news ISHU YA MWINYI ZAHERA KUWA MKALIMALI YANGA IPO HIVI

ISHU YA MWINYI ZAHERA KUWA MKALIMALI YANGA IPO HIVI


 KOCHA wa zamani wa Yanga ambaye kwa sasa ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Soka la Vijana ndani ya klabu hiyo, Mwinyi Zahera, amefunguka kwamba hajarudi Yanga kwa ajili ya kuwa mkalimani, bali ni kufanya kazi maalum aliyopewa na uongozi.

Akizungumza na Spoti Xtra, Zahera alisema: “Watu wanafikiri kuwa pengine nimekuja kufanya kazi ya ukalimani ndani ya Yanga kwa sababu nafahamu kuzungumza Kifaransa na Kiswahili, hapana, mimi nimepewa kazi maalum Yanga kuhakikisha soka la vijana linakua na kuleta faida ndani ya timu.

“Yanga ili iweze kupata mafanikio lazima ipitie katika mifumo ya kisasa ikiwa ni pamoja na kuinua soka la vijana, naamini nitafanikiwa ndani ya Yanga kwa kuwa kuna vipaji vingi sana hapa nchini na vitaenda kuinufaisha klabu hii,” .

Tayari Zahera ambaye aliwahi kufanya kazi ndani ya Yanga akiwa ni Kocha Mkuu kabla ya kibarua chake kusitishwa ameanza kazi na yupo ndani ya kikosi hicho ambacho kimetwaa taji la Ngao ya Jamii.


SOMA NA HII  KUELEKEA MICHUANO YA CAF MSIMU UJAO...YANGA KUPANGWA NA VIGOGO HIVI VYA SOKA...WASIPOJIPANGA IMEKULA KWAO...