Home Uncategorized AZAM FC: MAPAMBANO BADO YANAENDELEA, AKILI ZETU SASA NAMUNGO

AZAM FC: MAPAMBANO BADO YANAENDELEA, AKILI ZETU SASA NAMUNGO


AGREY Morris, nahodha wa Azam FC amesema kuwa kushindwa kupata ushindi mbele ya Ndanda sio mwisho wa mapambano kwani bado wana mechi mkononi.

Azam FC jana, Februari 18 ilikubalili sare ya kufungana bao 1-1 na Ndanda kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

“Haina maana kushindwa kupata ushindi mbele ya Ndanda ni mwisho wa mapambano, bado kuna kazi ya kufanya ambayo inaendelea, mashabiki watupe sapoti.

“Mchezo wetu unaofuata dhidi ya Namungo tutapambana kupata matokeo mazuri,” amesema. 

Bao la Ndanda lilifungwa na Vitalis Mayanga dakika ya 10 na lile la Azam FC lilifungwa na Andrew Simchimba.

SOMA NA HII  SUALA LA VAR AFRIKA NI PASUA KICHWA