Home news SABABU YA KAMBI YA YANGA ARUSHA KUFUTWA IPO HIVI

SABABU YA KAMBI YA YANGA ARUSHA KUFUTWA IPO HIVI


 YANGA watabaki kwenye kambi yao iliyopo Avic 
Town Dar baada ya uongozi kuamua kufuta ratiba ya kwenda kuweka kambi Arusha kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya Ligi Kuu Bara.

Uongozi wa Yanga umeshtukia ratiba yao ya kuweka kambi Karatu wakiona ni kama watapoteza muda kwa kuwa muda uliobaki ni mchache na itakuwa vizuri kama wakibaki Dar na kuepusha gharama zisizo na msingi.

Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Thabity Kandoro, ameliambia Championi Ijumaa: “Timu itabaki Dar es salaam ikiwa kwenye kambi yetu ya Avic Town, baada ya kufikia uamuzi wa kusitisha safari ya kwenda Arusha kuweka kambi.

“Kubaki hapa kutaipa timu nafasi ya kupumzika na kuwapunguzia uchovu wa safari za hapa na pale, lakini pia hapo kuna ishu ya gharama.”

Yanga inajiandaa na mechi ya tatu ya Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC itakayopigwa Uwanja wa Majimaji, Songea mkoani Ruvuma Oktoba 19 na sasa wamekuwa wakitenga muda wa kuingia Gym.

Leo Oktoba 10 inatarajiwa kuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya JKU SC unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, saa 1:00 usiku.


SOMA NA HII  TRY AGAIN: KUJIUZULU KWA BARBARA NI UPEPO MBAYA...SIMBA NI TIMU KUBWA AFRIKA...