Home Yanga SC ALIYEWATUNGUA SIMBA AFUNGUKA KUWA WALIKUWA NA JAMBO

ALIYEWATUNGUA SIMBA AFUNGUKA KUWA WALIKUWA NA JAMBO

 ZAWAD Mauya, kiungo wa Yanga amesema kuwa walikuwa na jamboao ambalo walipanga muda mrefu wanafurahi kuona limetimia.

Nyota huyo jana, Julai 3 aliibuka shujaa baada ya kupachika bao pekee la ushindi mbele ya watani wa jadi, Simba.

Wakati ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 0-1 Yanga, zawadi hiyo kwa mashabiki ilipatikana dk ya 12 kutoka kwa mguu wa Mauya.

Mauya amesema:”Tulikuwa tuna jambo letu ambalo tulipanga tangu awali kulifanya na jambo lenyewe ilikuwa ni ushindi.

“Kwa kilichotokea kwetu ni furaha na tunaamini kwamba mashabiki wamepata kile ambacho walikuwa wanastahili, ” amesema.

Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha pointi 70 nafasi ya pili huku Simba ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 73.


SOMA NA HII  WACHEZAJI YANGA WAOGA MINOTI