Home Simba SC MANULA APEWA MAJUKUMU YA UKOCHA WA MAKIPA SIMBA

MANULA APEWA MAJUKUMU YA UKOCHA WA MAKIPA SIMBA


KUFUATIA kukosekana kwa kocha wa makipa wa Simba, Milton Nienov aliyepata matatizo ya kifamilia, mlinda mlango namba moja wa kikosi hicho, Aishi Manula ndiye amebebeshwa mikoba ya ukocha wa makipa, kwa kuongoza mazoezi ya makipa wa timu hiyo wakati wa maandalizi ya mchezo wao wa juzi jioni dhidi ya Yanga. 

Kocha Nienov alikosekana kwenye mchezo wa jana dhidi ya Yanga kufuatia kuondoka kwa ruhusa maalum, ya kushughulikia masuala ya kifamilia kwao nchini Brazili.

Katika mazoezi ya Simba ambayo tuliyashuhuhudia Manula alionekana kuchukua jukumu la kuongoza programu za mazoezi hayo kwa kuwaongoza wenzake, Beno Kakolanya na Ally Salim.

SOMA NA HII  TAKWIMU ZINAONGEA.....MPAKA SASA CHAMA HOI KWA FEI TOTO...KAACHWA MBALI SANA...