Home Simba SC SABABU ZA SIMBA KUMRUDISHA CHIKWENDE ZIMBABWE ZATAJWA

SABABU ZA SIMBA KUMRUDISHA CHIKWENDE ZIMBABWE ZATAJWA

 


IMEFICHUKA kuwa benchi la ufundi la Simba limemrudisha Zimbabwe kiungo mshambiliaji wao, Perfect Chikwende kwa ajili kumsaidia kupata muda mwingi zaidi wa kucheza kwenye kikosi cha timu yao ya Taifa inayojiandaa na michuano ya COSAFA, kwa lengo la kumrudishia utimamu wa mwili.

Chikwende alisajiliwa na Simba katika kipindi cha dirisha dogo la usajili kutokea ndani ya kikosi cha Platinum ya Zimbabwe, mara baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika michezo miwili ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba.

Tangu atue Simba Chikwende aliyekuwa akipewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri, amekuwa akipata wakati mgumu kuingia ndani ya kikosi cha kwanza, na kupelekea kuwepo na taarifa kuwa huwenda Simba wakafanya maamuzi ya kuachana na kiungo huyo au kumtoa kwa mkopo mwishoni mwa msimu huu.

Akizungumzia mpango huo kocha mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema: “Ni kweli benchi la ufundi limeamua kumrudisha Chikwende Zimbabwe, kuungana na kikosi cha timu ya Taifa ya nchi hiyo inayojiandaa na mashindano ya COSAFA.

“Tumefanya hivi kama sehemu ya programu maalum ya kumpa Chikwende muda mwingi zaidi wa kucheza, na kuzidi kuimarisha utimamu wake wa mwili, na Bila shaka kama atazingatia programu tuliyompa basi atarejea akiwa bora zaidi.

SOMA NA HII  KUHUSU USAJILI WA CHAMA..SIMBA WATOA TAARIFA MPYA...AHMED ALLY AFICHUA 'CODE'...