Home kimataifa ROMELU LUKAKU ANA TUZO MBILI ZA UFUNGAJI BORA

ROMELU LUKAKU ANA TUZO MBILI ZA UFUNGAJI BORA


ROMELU Lukaku, raia wa Ubelgiji alijiunga na Klabu ya Inter Milan inayoshiriki Seria A, Agosti 8,2019 na mkataba wake unatarajiwa kumeguka Juni 30,2024 lakini utavunjwa na mabosi wa Chelsea ambao inaelezwa kuwa watamsajili mchezaji huyo kwa dau la pauni milioni 97.5.

Usajili wa Lukaku ambaye aliletwa duniani Mei 13, 1993 unaingia kwenye rekodi za sajili ghali England ambapo atakuwa anashika namba mbili kwa wachezaji waliosajiliwa kwa bei ghali.

Namba moja kwa sasa ni Jack Grealish kiungo ambaye ni mali ya Manchester City ambapo aliibuka huko akitokea Aston Villa na dau lake ni pauni milioni 100 ukiwa ni usajili ghali zaidi.

Ana tuzo mbili za ufungaji bora ambapo alitwaa msimu wa 2014/15 katika Europe League akiwa ndani ya Everton alitupia mabao 8 pia alisepa na tuzo ya ufungaji bora msimu wa 2009/10 wa Jupiler Pro League alitupia mabao 15.

Msimu wa 2020/21 ni mchezaji bora wa mwaka ndani ya Inter Milan ambayo ilitwaa ubingwa pia wa Seria A. Taji lake lingine ni lile la FA Cup alitwaa akiwa ndani ya Chelsea msimu wa 2012 akiwa ndani ya RSC Anderlecht msimu wa 2009/10 alitwaa taji la Ubelgiji.


SOMA NA HII  MOURINHO AVUNJA UKIMYA AWACHANA MAN U..."SIKUPEWA SAPOTI NA UONGOZI...AMEONGEA HAYA