Home Uncategorized YANGA: SIBOMANA, BALINYA WATATUFIKISHA MBALI KITAIFA NA KIMATAIFA

YANGA: SIBOMANA, BALINYA WATATUFIKISHA MBALI KITAIFA NA KIMATAIFA


MWINYI Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa kasi ya Patrick Sibomana raia wa Rwanda ya kushuka na kupandisha mashambulizi itawabeba kitaifa na kimataifa.
Zahera amesema kuwa kasi ya winga huyo sambamba na wachezaji wengine ambao wamesajiliwa kwa sasa akiwemo Juma Balinya inampa matumaini ya kufanya vizuri kutokana na kutibu tatizo ambalo alikuwa nalo msimu uliopita.
“Timu ya msimu uliopita ina tofauti sana na hii ambayo ninayo kwa sasa. Msimu uliopita ilikuwa kwamba kama ikitokea timu inapoteza mpira basi inakuwa shida kwa sababu wachezaji wanatembea tu.

“Lakini kwa wachezaji wapya hawa utaona kama wanashambulia basi wanapanda wengi lakini kama tunapoteza mpira basi wanakimbia haraka kuja kukaba. Kwa aina ya watu hawa ambao nilikuwa ninawataka nina uhakika mkubwa kwamba tutafanya vizuri kwenye msimu huu,” amesema.

Yanga ina kibarua mbele ya Township Rollers kati ya Agosti 23-25 ugenini baada ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 uwanja wa Taifa
SOMA NA HII  MASHABIKI UINGEREZA KUPEWA RUKSA YA KUINGIA UWANJANI