Home Simba SC SIMBA BANA..WASAJILI STRAIKA ‘ALIYESHINDWA KAZI’ TUNISIA..GOMES AFUNGUKA

SIMBA BANA..WASAJILI STRAIKA ‘ALIYESHINDWA KAZI’ TUNISIA..GOMES AFUNGUKA


SIMBA iko kwenye hatua nzuri ya kumalizana na straika Mghana, Abdul Basit Khalid aliyeachana na Esperance ya Tunisia . Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba iliyofika jana kambini nchini Morocco, mchezaji huyo kama dili likikamilika ataungana nao juu kwa juu.

Khalid ametemana na Esperance kama ilivyokuwa kwa mkongomani wa Yanga, Heritier Makambo aliyeachana na Horoya ya Guinea akarudi Jangwani kuendeleza alipoishia.

Habari za uhakika zinasema Mghana huyo mwenye rasta, machachari ndiye anayepewa nafasi kubwa na benchi la ufundi ingawa pia Mkongomani, Kadima Kabangu nae ameshakubaliana mambo mengi na viongozi na wamemwambia akae mkao wa safari.

Kabangu anayemaliza mkataba wake wa DCMP ya DR Congo ameshawaambia marafiki zake anakuja Tanzania kukipiga na Simba na walimalizana wikiendi iliyopita.

Habari zinasema Didier Gomes ambaye ni raia wa Ufaransa, anaukubali zaidi aina ya uchezaji wa Khalid na uzoefu wake kimataifa jambo ambalo linaweza kuwabeba Simba msimu ujao unaoanza Septemba 11.

Staa huyo alijiunga na Esperance Januari 2021 lakini alishindwa kutamba kama benchi la ufundi lilivyokuwa limemtarajia, lakini Simba wanaamini mfumo wa Watunisia hao ulimfelisha. Mchezaji huyo anajiunga na Simba huku kukiibuka sintofahamu ndani ya usajili wa Simba baada ya jana Meddie Kagere, Perfect Chikwende walioko kwenye orodha ya kuachwa waliposafiri na timu kwenda kambini kujiandaa na msimu mpya.

SOMA NA HII  FIFA WAMZUIA KAGERE KUCHEZA SIMBA SC