Home Yanga SC KOCHA MHOLANZI AFUNGUKA ISHU YA KUWAPELEKA YANGA FIFA

KOCHA MHOLANZI AFUNGUKA ISHU YA KUWAPELEKA YANGA FIFA

 


ALIYEKUWA kocha wa Yanga, Mholanzi Hans Van Der Pluijm amethibitisha kuwa kuna uwezekano mkubwa akaifungulia mashitaka klabu ya Yanga kwa Shirikisho la soka la Kimataifa FIFA, kuhusiana na madai ya stahiki zake.

Inaelezwa kuwa kocha huyo anawadai Yanga kiasi cha Dola za Kimarekani 50,000 ambazo ni sawa na Shilingi Milioni 115 za Kitanzania.

Pluim, aliiongoza Yanga kama kocha mkuu kwa vipindi viwili tofauti kuanzia mwaka 2014 hadi 2017, huku pia akiwahi kushika nyazifa nyingine ndani ya klabu hiyo.

Akizungumza na Championi Jumatano, Pluijm alisema: “Taarifa za mimi kuwa kwenye mpango wa kuwapeleka Yanga FIFA ni za kweli, lakini nisingependa kuzungumza sana kuhusu suala la kesi hii kwa sasa, kwa kuwa kuna wawakilishi wangu ambao wako Dar es Salaam kwa ajili ya kushughulikia kesi hii.”

Tulipomtafuta Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema: “Taarifa za kudaiwa na kocha Hans zinapaswa kuwekwa sawa kwa kuwa ni kweli alikuwa akitudai, lakini tayari suala hili lilishafanyiwa kazi.”

SOMA NA HII  HUKU HOMA YA PAMBANO LA WATANI LIKIZIDI KUPANDA....YANGA WAIKIMBIA SIMBA MWANZA...ISHU NZIMA IKO HIVI...