Home Yanga SC HATIMAYE KISINDA AFUNGUKA A-Z KUHUSU DILI LA KUTUA MOROCCO..AMTAJA MOLOKO

HATIMAYE KISINDA AFUNGUKA A-Z KUHUSU DILI LA KUTUA MOROCCO..AMTAJA MOLOKO


STAA aliyeuzwa na Yanga kwenye kikosi cha Berkane ya Morocco, Tuisila Kisinda amewaambia Yanga; “Msiwe na wasiwasi, Moloko yuko vizuri.”

Kauli hiyo ya Tuisila imekuja saa chache huku mashabiki wa Yanga wakiwa na wasiwasi hatua ya klabu yao kumuuza wameharibu.

Tuisila maarufu kama TK Master mwenyewe amesisitiza  anayekuja naye ni moto kama yeye wala hana wasiwasi na kiwango chake.

Kisinda ambaye ni raia wa DR Congo, ametua jana nchini Morocco tayari kwa kumalizana na klabu ya RS Berkane ya huko inayofundishwa ana kocha wa zamani wa AS Vita Florent Ibenge wakiwahi kufanya kazi pamoja na winga huyo.

Kisinda amesema anakwenda kutafuta changamoto mpya na hana wasiwasi na winga Jesus Moloko anayetua Yanga kuziba nafasi yake kwani jamaa hana tofauti naye kubwa kwavile wanajuana kiuchezaji.

Alisema anamjua vyema Moloko kutokana na kufanya kazi naye pamoja na kwamba ubora wake ndio ulikuwa unawafanya kupishana na kushindania namba vizuri wakiwa Vita na ilikuwa ni kazi kazi.

“Moloko ni mchezaji mzuri sana, mashabiki wala wasidhani kuna kitu kitapungua ataendeleza pale nilipoishia namjua vizuri nimecheza naye tukiwa Vita naona klabu imepata mtu sahihi sana,” alisema Kisinda.

“Anajua kama mimi tukiwa pale Vita ndio maana kocha alikuwa akitupa nafasi tofauti kama yeye anaanza mimi nitasubiri au kama mimi nitaanza yeye anasubiri na sasa amekomaa vizuri,” alisema Tuisila ambaye alikuwa akisifika kwa mbio.

Kisinda alinogesha mabeki wasidhani kuna kitu kitapungua Yanga kwa kuwa Moloko naye ana kasi kama ilivyokuwa yeye ambapo sasa jambo zuri Yanga ni kwamba atatua akikutana na mastraika wazuri wa kutupia.

Aliongeza mashabiki watulie na wamwamini Moloko watafurahi kwa kazi ambayo atawafanyia huku akisifu pia usajili wa timu yake hiyo kuelekea msimu ujao ambao ametamba kwamba itakuwa Yanga ya aina yake.

“Ana kasi sana (Moloko) ni mtu kama mimi tu mabeki wasifikiri Yanga kasi imepungua… tena najua Moloko atawakimbiza sana na mashabiki wa Yanga watafurahi,kitu kizuri sasa atafika pale kukiwa na washambuliaji wazuri.

SOMA NA HII  YANGA YAPIGIA HESABU UBINGWA WA SIMBA

“Timu ya Yanga sasa wamefanya usajili mzuri sana,kabla sijaondoka nilikutana na bosi mkubwa wa GSM akaniambia anataka kutengeneza timu bora sana kwa msimu ujao na sasa naona kutakuwa na moto pale,” aliongeza Tuisila ambaye muda wowote anaweza kutambulishwa na kuanza kujinoa Morocco.

Tuisila ni miongoni mwa mastaa waliowakosha mashabiki wa Yanga hususani kasi yake kwenye dabi ya Kariakoo alivyokuwa akikimbia na chaki.