Home Yanga SC YANGA KUMSAJILI BEKI HUYU WA SIMBA

YANGA KUMSAJILI BEKI HUYU WA SIMBA

 IMEELEZWA kuwa mabosi wa Yanga wapo kwenye hesabu za kuinasa saini ya beki aliyeachwa Simba, Peter Muduhwa.

Raia huyo wa Zimbabwe alitangazwa kuwa mali ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes na sababu kubwa ilikuwa ni kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika. 

Haikuwa hivyo kwani nyota huyo alisepa Bongo akiwa hajacheza mchezo hata mmoja katika Ligi ya Mabingwa Afrika na Simba iliishia hatua ya robo fainali.

Chanzo kutoka ndani ya Yanga kimeeleza kuwa Yanga wamefanya mazungumzo ya awali na beki huyo ikiwa hakutakuwa na mabadiliko basi anaweza kusaini dili jipya.

Yanga kwa sasa ipo kwenye maboresho ya kikosi ambapo Kamati ya Usajili inaongozwa na Injinia Hersi Said ambaye ni Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo ambayo imeshamalizana na baadhi ya nyota ikiwa ni pamoja na Heritier Makambo,  Dickson Ambundo. 


Chanzo: Championi

SOMA NA HII  BADO NI SIMBA, YANGA SASA NI KIGOMA UNAAMBIWA SIO POA