Home Habari za michezo BADO NI SIMBA, YANGA SASA NI KIGOMA UNAAMBIWA SIO POA

BADO NI SIMBA, YANGA SASA NI KIGOMA UNAAMBIWA SIO POA

KOCHA wa Mashujaa, Mohamed Abdallah ‘Baresi’ amesema kwa namna mashabiki wa Kigoma walivyo na hamu ya kuziona timu kama Simba, Yanga, Azam FC na nyingine anaona ana kazi ya kukiandaa kikosi kitakachowapa furaha.

Alisema kutokana na kukosekana timu ya Ligi Kuu kwa karibu miaka 20 mkoani humo ni sababu ya mashabiki kungojea kwa hamu msimu unaoanza Agosti 15.

“Huwa nawaambia wachezaji waangalie mzigo waliotishwa na mashabiki, kwani huwa wanasikia wanavyozungumza kila wanapokuja mazoezini, hiyo ni ishara ya kuhitaji furaha zaidi,” alisema Baresi na kuongeza;

“Mashabiki wana matumaini makubwa, baada ya muda mrefu kutoishuhudia Ligi Kuu sasa itakuwa muda wao wa kufurahia soka.”

Baresi alisema maandalizi kwa ujumla yapo vizuri, anaamini wataanza msimu mpya kwa mafanikio ya juu, huku akisisitiza anatambua itakuwa ligi yenye ushindani mkubwa, kulingana na sajili zilizofanywa na timu.

“Timu zimesajili hivyo haitakuwa kazi rahisi katika kusaka pointi tatu, ila pamoja na hayo nakiamini kikosi changu kitafanya kazi nzuri, licha ya ugeni katika Ligi Kuu ”alisema.

Mashaujaa imepanda daraja msimu huu.

SOMA NA HII  AZIZ KI AWAPASUA KICHWA YANGA...WASHINDWA KUMTABIRI...SIMBA WASHANGAZWA