Home Habari za michezo AZIZ KI AWAPASUA KICHWA YANGA…WASHINDWA KUMTABIRI…SIMBA WASHANGAZWA

AZIZ KI AWAPASUA KICHWA YANGA…WASHINDWA KUMTABIRI…SIMBA WASHANGAZWA

Habari za Yanga SC

Stephane Aziz Kl ni mchezaji asiyetabirika kwa kweli na anatuchanganya sana.

Kuna wakati huwa hachezi vizuri na hadi anawapa hofu waliomsajili kujihisi kama wamepigwa kwa hela nyingi walizotoa kumnasa.

Hili sidhani kama tunaweza kubishana kwani hata kocha Nasreddine Nabi kuna wakati aliwahi kumtoa mapema tu uwanjani akidai hakuridhishwa na kiwango chake.

Lakini ghafla anaibukaga na kufanya vitu vya maana hadi watu mnasahau kiwango cha chini alichokionyesha siku za kabla ya mechi husika.
Mfano alipokuja hakuonekana akicheza vyema akaja kupiga bao kali la faulo dhidi ya Simba nchi nzima ikaanza kumuongelea yeye.

Akapotea kwa muda kisha akafunga dhidi ya Mtibwa Sugar na baada ya hapo akawapa raha Yanga kwa kufunga bao muhimu katika mechi ya kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ugenini dhidi ya Club Africain.

Kama kawaida yake akapotea tena na juzi kapiga hat trick dhidi ya Kagera Sugar tena wakiwa wanajiandaa kuikabili Simba keshokutwa.
Amekuwa kama uyoga yule mchezaji Kuna wakati unakuwa sumu na wakati mwingine unaliwa.

SOMA NA HII  UHAKIKA WA MKEKA WAKO KUTIKI LEO NI MKUBWA KUPITIA ODDS HIZI NDANI YA MERIDIANBET..