Home news POLISI TANZANIA WAANZA KUIVUTIA KASI SIMBA

POLISI TANZANIA WAANZA KUIVUTIA KASI SIMBA


 BAADA ya kupewa mapumziko ya siku nane
 kikosi cha Polisi Tanzania kimeingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba.

Polisi wanatarajia kuwakaribisha Simba Juni19, mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Wachezaji wa timu hiyo walipewa mapumziko baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi dhidi ya Coastal Union ambapo Polisi iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Hassan Juma alisema kuwa: β€œTimu ilianza mazoezi mapema wiki hii kwenye Uwanja wa TPC, Moshi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Simba.

β€œAskari wa mwamvuli wamerejea wakiwa na ari na morali ya kupambana ya kuhakikisha malengo ya timu kwa msimu huu ya kukusanya pointi 12 katika michezo iliyobaki ukiwemo ule wa Simba yanaweza kufikiwa.”

Polisi Tanzania imebakiwa na michezo minne kuelekea mwishoni mwa msimu huu, ikiwa ni dhidi ya Simba, Kagera Sugar, Mwadui na Ruvu Shooting, na ipo katika nafasi ya sita kwenye msimamo ikiwa na pointi 41.

SOMA NA HII  ISHU YA KAKOLONYA KUACHWA YAZUA JAMBO ...MASTAA SIMBA WATOA TAMKO HILI...