Home Habari za michezo PHIRI AITAKA NAMBA YAKE SIMBA…ATANGAZA JAMBO ZITO KWA KINA BOCCO…

PHIRI AITAKA NAMBA YAKE SIMBA…ATANGAZA JAMBO ZITO KWA KINA BOCCO…

Habari za Simba

Baada ya kukaa nje ya Uwanja kwa majuma kadhaa akiuguza majeraha, Straika wa Simba Moses Phiri amesema kwa sasa yuko fiti asilimia 100 kupambania namba yake aliokuwa anaanza kabla ya kukumbwa na majeraha.

Phiri ambae amefunga mabao 10 ya Ligi Kuu alikua ndio mshambuliaji Kinara wa Simba lakini alipata majeraha yaliyomfanya akae nje kwa majuma kadhaa.

Kwa sasa Phiri yuko fiti na amesema anahitaji muda wa kutosha kucheza kwa lengo lake ni kupambania namba.

“Kwa sasa nipo fiti nahitaji dakika nyingi ili niweze kufunga mabao, malengo yangu mwanzoni mwa msimu yalikuwa ni kufikisha zaidi ya mabao 15, nitahitaji muda wa kucheza ambao utanijengea kujiamini zaidi, tofauti na dakika chache ambazo zinakuwa na presha kubwa.”

SOMA NA HII  YANGA:-"FEI TOTO ACHA UJEURI...HUWEZI KUSHINDANA NA KLABU...ISHU NZIMA IKO HIVI A-Z