Home Azam FC MABOSI AZAM ‘WAKOPI NA KUPESTI’ YOTEE YA SIMBA….WAIGA ‘PLANI’ ZA KWENDA UARABUNI...

MABOSI AZAM ‘WAKOPI NA KUPESTI’ YOTEE YA SIMBA….WAIGA ‘PLANI’ ZA KWENDA UARABUNI KUJINOA…ISHU NZIMA IKO HIVI…


Matajiri wa soka nchini, Azam inatarajia kuifuata Simba nchini Misri kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya msimu ujao.

Habari kutoka ndani ya Azam zinasema kuwa, kambi ya maandalizi ya msimu imepangwa kuwa Misri ama Tunisia ikiwa ni pendekezo la benchi la ufundi linaloongozwa na Abdihamid Moallin.

Kama itaenda Misri itaungana na Simba iliyopanga nao kuweka huko kuanzia wiki ijayo, lakini ikiwa vipi watatua Tunisia kwa muda wa wiki zisizopungua mbili.

“Tunatarajia kuweka kambi sehemu nzuri na tulivu itakayowajenga wachezaji wetu kiakili na kimwili ila kwa sasa bado viongozi wanaendelea na taratibu zote za mwisho,” kilisema chanzo hicho ambacho hakikutaka kuwekwa wazi.

Nyota wa kikosi hicho wanatarajiwa kurejea kambini kuanzia Julai 20 na baada ya hapo wataanza kambi ya wiki moja Dar es Salaam kisha kwenda kati ya nchi hizo kujiandaa na msimu mpya unaotarajiwa kuanza Agosti 17.

Azam imeanza kuboresha kikosi wakisajili mastaa wapya Kipre Junior na Tape Edinho kutoka Ivory Coast, Isah Ndala ya Nigeria na wazawa akiwamo Abdul Sopu.

SOMA NA HII  HIVI NDIVYO SAKHO NA TUZO YAKE WALIVYOPOKELEWA MISRI NA MASTAA WA SIMBA...AMKIMBILIA KAPOMBE NA KUMKUMBATIA...