Home Yanga SC NINJA NAYE YUPO KWENYE ORODHA YA WATAKAOIKOSA NAMUNGO KESHO

NINJA NAYE YUPO KWENYE ORODHA YA WATAKAOIKOSA NAMUNGO KESHO


KESHO Uwanja wa Majaliwa, Namungo FC ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ikiwa ni mzunguko wa pili.

Mchezo wa kwanza, Yanga walikubali sare ya kufungana bao 1-1, Uwanja wa Mkapa na kufanya wagawane pointi mojamoja.

Katika mchezo huo Nassredine Nabi ambaye ni Kocha Mkuu wa Yanga atakosa huduma ya beki wa kati Abdala Shaibu, ‘Ninja’ ambaye anasumbuliwa na tatizo la misuli.

Ninja amekuwa kwenye ubora wake kwenye mechi za hivi karibuni ambapo alikuwa ni chaguo la kwanza la Nabi raia wa Tunisia.

Mbali na Ninja pia Yanga itakosa huduma ya Carlos Carlinhos ambaye ni kiungo mshambuliaji ambaye naye anasumbuliwa na tatizo la misuli.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa wachezaji hao wanaendelea na matibabu ili waweze kurejea kwenye ubora.

SOMA NA HII  MCHEZO MZIMA KWA YANGA KUIMALIZA MWADUI FC ULICHEZWA HIVI