Home Habari za michezo BAADA YA YANGA KUILALAMIKIA SIMBA KWA KUISUSA MECHI YA LEO…AHMED ALLY KAWAJIBU...

BAADA YA YANGA KUILALAMIKIA SIMBA KWA KUISUSA MECHI YA LEO…AHMED ALLY KAWAJIBU HAYA KIBABE…


Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amezijibu tuhuma za Watani zao wa jadi, Yanga kwamba Simba wamekaa kimya hawataki kuipigia promo mechi yao ya leo kwa kuwa mwenyeji ni Yanga hivyo atafaidika.

Hii inakuja baada ya Manara kudai kuwa hawezi kufanya promo kwa kutembea barabarani kuhamasisha kama ambavyo amekuwa akifanya Ahmed kwa Simba kwani hlevel hiyo alishatoka.

Aidha, kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema Simba wana roho mbaya kwani hawataki kuifanyia promo mechi hiyo wakiamini uwanja ukijaa Yanga atapata faida kutokana na makusanyo ya viingilio.

“Nilivyoambiwa tuchukue kalamu na karatasi tujifunze Promo fasta fasta nikaagiza Counter Book Quire 4 mwisho wa siku ooh Simba mna roho mbaya hamfanyi Promo sasa tutafanyaje promo wakati tunaandika yaan mnataka tuimbe huku tunapiga mluzi inawezekana vipi?

Sasa tukutane Benjamin Mkapa tukaoneshane kazi tunahamu sana na nyie,” amesema Ahmed.

SOMA NA HII  SIMBA vs PRISONS UWANJA WA MKAPA NI VITA YA KISASI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here