Home Simba SC KAGERE, BOCCO NA MUGALU WAMPA KIGUGUMIZI GOMES ISHU YA USAJILI

KAGERE, BOCCO NA MUGALU WAMPA KIGUGUMIZI GOMES ISHU YA USAJILI


 MABAO ambayo wameyafunga washambuliaji watatu wa Klabu ya Simba, John Bocco, Chris Mugalu na Meddie Kagere yamempa kigugumizi kocha mkuu wa timu hiyo, Didier Gomes kuhusiana na usajili wa mshambuliaji mpya ndani ya kikosi hicho.

 

Safu ya ushambuliaji ya Simba imewea kuonyesha makali kwa msimu wa 2020/21 ambapo imeweza kuwafanya wote watatu kufunga zaidi ya mabao 10.


Ni mabao 16 ya Bocco, akifuatiwa na Mkongomani Chris Mugalu mwenye mabao 15, huku mfungaji bora wa misimu miwili mfululizo iliyopita Meddie Kagere yeye akiwa ameweka kambani mabao 13.

 

Simba imekuwa ikihusishwa na usajili wa baadhi ya majina makubwa ya washambiuliaji wakiwemo Walter Bwalya wa Al Ahly, Kadima Kabangu wa DC Motema Pembe na Emmanuel Okwi.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, kuhusu usajili wa straika mpya ndani ya kikosi hicho Gomes alisema: “Kwanza ningependa kuweka wazi kuwa nina furaha kubwa na ubora wa washambiuliaji wote watatu walio ndani ya kikosi changu.

 

“Kuhusu ikiwa tunahitaji kusajili mshambuliaji mpya msimu ujao, inawezekana likawa ni wazo zuri lakini siwezi kusema tuna ulazima sana wa kufanya hivyo.”

SOMA NA HII  KOCHA WA SIMBA AFURAHI KUPATA SAINI YA ONANA, AFUNGUKA MPANGO WAKE