Home Habar za Usajili Simba BAADA YA KUMALIZANA NA SIMBA…KAPAMA AWAPIGA ‘MKWARA WA KWENDA’ MASTAA WENZAKE MSIMBAZI…

BAADA YA KUMALIZANA NA SIMBA…KAPAMA AWAPIGA ‘MKWARA WA KWENDA’ MASTAA WENZAKE MSIMBAZI…


Rasmi klabu ya Simba imepata saini ya kiungo mshambuliaji, Nassoro Kapama aliyesajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili kutoka Kagera Sugar, huku akichimba mkwara kwamba ametua Msimbazi kwa kazi moja tu.

Kapama alisema licha ya kutua timu yenye ushindani mkubwa, lakini anajivunia kumudu kwake kucheza zaidi ya nafasi moja, kitu anachoamini kitambeba Msimbazi.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Kapama alisema malengo yake ya kucheza Simba yametimia kwani ilikuwa ni ndoto ya muda mrefu hivyo anaenda kuiishi huku akisema yupo tayari kupambana kwa ajili ya nafasi yake.

“Nawashukuru viongozi wa Simba kwa kuonyesha imani kubwa kwangu, haikuwa rahisi ila ninachoweza kuwaahidi ni kuwapa furaha iliyowafanya kunileta hapa, naamini tutafikia malengo kwa pamoja,” alisema Kapama na kuongeza;

“Unapocheza timu kama Simba lazima ukutane na ushindani kwa sababu unakutana na wachezaji tofauti tofauti, ila hilo kwangu siliwazii au kuangalia fulani alifeli bali ni kupambana kadri ya uwezo wangu wote.”

Aliongeza anawashukuru pia viongozi na mashabiki wa Kagera kwa sapoti aliyopata katika kipindi chote cha misimu miwili alichowatumikia huku akisema wataendelea kubaki watu muhimu katika safari yake hiyo mpya.

Nyota huyo yupo jijini, Dar es Salaam maeneo ya Chamazi alikofikia na muda wowote kuanzia sasa atatambulishwa kama mchezaji mpya akiungana na Yusuph Mhilu aliyetokea pia Kagera Sugar msimu uliopita.

Kapama ambaye husifika kwa uwezo wake wa kucheza nafasi nyingi uwanjani alifunga mabao mawili na kuwezesha matatu (asisti) msimu uliopita ukiwa ni usajili wa tatu kwa Simba baada ya Habib Kyombo (Mbeya Kwanza) na Moses Phiri kutoka Zanaco ya Zambia.

SOMA NA HII  NAMUNGO KUIVURUGA YANGA, KAZE AMFANYIA UMAGIA GAMONDI