Home Uncategorized MWANA FA:NIMEPONA CORONA, WADUDU WALINING’ANG’ANIA

MWANA FA:NIMEPONA CORONA, WADUDU WALINING’ANG’ANIA


HAMISI Mwinjuma maarufu kama Mwana FA mwimbaji wa Bongo Fleva, amesema kuwa kwa sasa tayari amepona maambukizi ya Virusi vya Corona alivyokuwa anauguza.

FA alikuwa miongoni mwa wagonjwa wa mwanzo kabisa kujitangaza kupitiaukurasa wake wa Istagram kuwa amepata maambukizi hayo na alijitenga kwa muda na familia yake kabla ya kuwa chini ya uangalizi wa Serikali.

FA amesema:”Nimekaa siku 28 kwenye isolation, nimepimwa mara 8 hadi kupatikana negative, mara zote nilizopimwa nilikuwa napatikana positive na ukipatikana positive wanakaa masaa 72 hadi kukupima tena! Naweza kusema ni kama huyu mdudu alining’ang’ania”,” amesema.


SOMA NA HII  WACHEZAJI SIMBA WAGOMA KISA MPUNGA