Home Habari za michezo MAYELE PAMOJA NA MASTAA HAWA WA YANGA KUKOSEKANA KESHO DHIDI YA TZ...

MAYELE PAMOJA NA MASTAA HAWA WA YANGA KUKOSEKANA KESHO DHIDI YA TZ PRISONS…

Tetesi za Usajili Yanga

KUELEKEA kwenye mchezo wa kesho wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons kuna baadhi ya nyota wa Yanga ambao wataukosa mchezo huo.

Kwa mujibu wa Cedrick Kaze, kocha msaidizi wa Yanga amesema kuwa wapo ambao wataukosa mchezo huo kutokana na sababu mbalimbali.

β€œDickson Job ana adhabu hatakuwepo kwenye mchezo wa kesho, Jesus Moloko na Mayele hawajafanya mazoezi tutawaangalia kwenye mazoezi ya leo kama watatumika kwenye mchezo wa kesho.

β€œBernard Morrison na Bakari Mwamnyeto wamerudi mazoezini lakini bado hawako vizuri asilimia mia moja,”.

Yanga ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 32 baada ya kucheza mechi 13 mchezo wake uliopita ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Ihefu ya Mbeya.

SOMA NA HII  GAMONDI AWAFANYIA UMAFIA WAARABU