Home Habari za michezo GAMONDI AWAFANYIA UMAFIA WAARABU

GAMONDI AWAFANYIA UMAFIA WAARABU

Habari za Yanga

Kikosi cha Yanga kinahesabu saa tu kabla ya leo jioni kuanza safari kuwafuata wapinzani wao, Al Merrikh lakini kuna hesabu za kimafia zimepigwa na mabosi wa timu hiyo wakishirikiana na kocha wao Miguel Gamondi.

Yanga imefanya hesabu za maana ikiwatuma watu wawili Rwanda ambao hadi leo wanamaliza siku ya nne nchini humo wakifanya kazi maalum kwa wapinzani wao.

Unavyosoma TanzaniaWeb.com muda huu pale Rwanda kocha msaidizi wa Gamondi, Moussa N’daw yupo Kigali akiwasoma El Merreikh kwenye mechi mbili za kirafiki wanazocheza.

Kazi hiyo ya N’daw ni kama kete muhimu kwa Yanga ambao kwa sasa washindwe wenyewe kwani wana kila kitu kuhusu wapinzani wao hao ambao watakutana nao Septemba 16 pale jijini Kigali Uwanja wa Pele kwenye mchezo wa hatua ya mtoano wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mapema Gamondi na mabosi wake walishatangulia kunasa mikanda miwili ya mechi mbili za Waarabu hao walipokuwa wanapambana na Otoho D’oyo wa Congo Brazzaville na Al Merrikh ilivuka hatua hiyo.

Mbali na N’daw pia Yanga ilimtanguliza meneja wa timu hiyo Walter Harrison kwa kazi maalum ya kuandaa hesabu za makazi ya timu yao ambayo itaondoka kesho Septemba 14 saa 11 jioni tayari kwa mchezo huo.

Yanga haitaki kufanya makosa yoyote eneo hili wakitambua wamewahi kukwama mara mbili kutinga makundi na waliangukia Kombe la Shirikisho Afrika nafasi ambayo msimu huu hawataipata baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kusitisha mbeleko hiyo.

Huku Tanzania Gamondi amebaki na wasaidizi wake wawili kocha wa makipa wa timu hiyo na kocha wa mazoezi ya viungo wakiendelea kujiandaa na mechi hiyo.

SOMA NA HII  BANGALA AFUNGUA KILA KITU, KUHUSU KUTUA AZAM, AWATAJA MAXI, SKUDU, TUHUMA ZAKE NA SIMBA