Home Habari za michezo BAADA YA KUFUNGWA NA YANGA LEO….KIBARUA CHA PABLO KIPO REHANI SIMBA….MUDA WOWOTE...

BAADA YA KUFUNGWA NA YANGA LEO….KIBARUA CHA PABLO KIPO REHANI SIMBA….MUDA WOWOTE ‘KITANUKA’ HUKOO…


YANGA imetinga fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba huku ikizidi kuhatarisha kibarua cha kocha Pablo Franco baada ya kumaliza msimu bila kufikia lengo hata moja alilowekewa na klabu.

Bao pekee la ushindi ambalo limeipekeka Yanga fainali limefungwa na kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ kwa shuti kali dakika ya 25 na kudumu kwa dakika zote 90 za mchezo huo.

Mchezo huo wa nusu fainali umepigwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo Yanga imezima ndoto za Simba kutetea kombe hilo.

Tayari Yanga wana uhakika wa asilimia 99 kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC hivyo matumaini pekee ya Simba kufuta machungu yalibaki kwenye michuano hiyo hivyo kung’olewa kwake leo kwenye mchezo wa nusu fainali kumezima ndoto zao.

Yanga ilimaliza dakika 45 za kipindi cha kwanza ikongoza kwa bao na kutawala mchezo hususani eneo la kiungo lililoongozwa na Khalid Aucho, Yanick Bangala, Feisal Salum na Salum Abubakar ‘Sure Boy’.

Simba imekianza kipindi cha pili kwa nguvu baada ya kufanya mabadiliko ya mapema ya wachezaji akitoka Thadeo Lwanga na kuingia Rally Bwalya ingizo ambalo limeleta nguvu mpya kwenye eneo la mwisho la Simba na kuanza kutengeneza mashambulizi.

Simba imefafanya mabadiliko mengine akiingia Yusuph Mhilu, Meddie Kagere na Erasto Nyoni wakichukua nafasi za Mzamiru Yassin, Kibu Denis na Jimmyson Mwanuke ambao kushindwa kuendelea na mchezo kutokana na majeraha.

Yanga imefanya mabadiliko ikiwatoa Kibwana Shomari aliyepata majeraha nafasi yake ikachukuliwa na Farid Mussa, Makambo akampisha Crispin Ngushi huku Feisal akimpisha Zawadi Mauya.

Mabadiliko hayo hayakubadilisha chochote kwani bao pekee lililofungwa na Fei Toto katika kipindi cha kwanza ndilo limedumu kwa dakika 90 na kuipeleka Yanga fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam.

Yanga itasubiri mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya Azam na Coastal Union itakayochezwa kesho katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ambapo fainali itapigwa baadae katika uwanja huo.

SOMA NA HII  KUHUSU TAARIFA YA TAIFA STARS vs UGANDA KUPIGWA USIKU SANA...UHAKIKA HUU HAPA...