Home Habari za michezo YANGA HII SASA TOO MUCH

YANGA HII SASA TOO MUCH

Habari za Yanga leo

Wakati matokeo ya msimu uliopita ya kutolewa Ligi ya Mabingwa Afrika na Al Hilal ya Sudan yakimuumiza kichwa, Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Angel Gamondi, mabasi takriban 50 imeelezwa tayari yamejaa kwa ajili ya kupeleka mashabiki wa Yanga jijini Kigali, Rwanda kwenda kuisapoti timu yao dhidi ya AlMerrikh.

Yanga ambayo msimu uliopita ilitolewa na Al Hilal katika mechi ya raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, msimu huu inakutana tena na Al-Merrikh ya Sudan pia kwenye raundi ya kwanza, jambo ambalo Gamondi anataka kuandika rekodi ya kuwatoa Wasudan hao.

Hata hivyo, tofauti na msimu uliopita ambao Yanga ilianzia nyumbani kabla ya biashara kwenda kuishia Sudan, msimu huu imepata bahati ya kuanzia ugenini na tena timu zote ni kama zipo ugenini kwani AlMerrikh inachezea mechi zake za nyumbani nchini Rwanda kutokana na Sudan kuwa katika machafuko ya kisiasa.

Akizungumza nasi, Gamondi alisema wanaendelea na maandalizi ya mwisho ya michezo ya hatua ya mtoano, anafahamu msimu uliopita walitolewa katika hatua kama hiyo na Al Hilal ya Sudan.

Alisema anajua ni muda mrefu Yanga haijacheza hatua ya makundi hali ambayo kuna ugumu lakini muhimu ni kuwa makini katika michezo miwili dhidi ya Al-Merrikh.

“Tumejipanga kuweka rekodi na historia mpya msimu huu, malengo yetu ni kuhakikisha tunafuzu makundi na kufika mbali zaidi kwani tunaamini kwenye ubora wa kikosi tulichonacho.

“Tunatakiwa kuwa makini na kuhakikisha tunashinda mechi zote mbili dhidi ya Al-Merrikh, ugenini na nyumbani ili tuendelee kusonga mbele na mashindano, tukipoteza hapa tutakuwa tumeaga mashindano jambo ambalo sitaki kuliona,” alisema Gamondi.

Alisema amefanikiwa kuona baadhi ya video za mechi walizocheza Al-Merrikh na amefanyia kazi ubora na madhaifu ya wapinzani wao, hivyo anatambua utakuwa mchezo wa ushindani kwa sababu ya rekodi ya mechi ya msimu uliopita kutolewa na Al Hilal kutoka Sudan.

Wakati Gamondi akieleza hayo, Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe, alisema kikosi chao kimeingia kambini jana kwa wachezaji walikuwapo katika majukumu ya timu zao za taifa kasoro wachezaji wawili, Djigui Diarra na Stephane Aziz Ki.

Kuhusu msafara wa mashabiki kuelekea nchini humo, Kamwe alisema wamepokea taarifa kutoka matawi mbalimbali ya Dar es Salaam na mikoa mingine na hadi sasa takriban mabasi zaidi ya 50 tayari wamethibitishiwa kuwa yatakwenda nchini humo.

Alisema kwa Dar es Salaam tu jumla ya mabasi 13 yataondoka hapa Alhamisi kuelekea Kigali, Rwanda yakiwa yamejaa mashabiki na mengine yatatoka mikoa mingine tofauti kuelekea nchini humo. Endapo Yanga itafuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, itakuwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 24 sasa.

SOMA NA HII  ALLY KAMWE: MAYELE ANASEPA YANGA....TIMU KUBWA DUNIANI ZINAMTAKA LEO KESHO...