Home Habari za michezo ALLY KAMWE: MAYELE ANASEPA YANGA….TIMU KUBWA DUNIANI ZINAMTAKA LEO KESHO…

ALLY KAMWE: MAYELE ANASEPA YANGA….TIMU KUBWA DUNIANI ZINAMTAKA LEO KESHO…

Habari za Yanga

UONGOZI wa Yanga, umeweka wazi kuwa, umepokea ofa nyingi kutoka timu mbalimbali zinazohitaji huduma ya nyota wao, Fiston Mayele raia wa DR Congo.

Mayele mkononi ana tuzo mbili za Ufungaji Bora, moja ya Ligi Kuu Bara 2022/23 baada ya kufunga mabao 17, nyingine ya Kombe la Shirikisho Afrika 2022/23 akifunga mabao 7.

Mshambuliaji huyo anatajwa kuwa kwenye hesabu za kuibukia Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, lakini pia anatajwa kuwaniwa na Sepahan FC ya nchini Iran.

Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, amesema kuna ofa nyingi ambazo wamepokea kutoka timu mbalimbali ambazo zinahitaji huduma ya Mayele.

“Ipo wazi kuwa kuna ofa nyingi ambazo tumepokea zikihitaji huduma ya mchezaji wetu Mayele, lakini kwa sasa bado ni mchezaji wa Yanga na yupo kwenye majukumu ya timu ya taifa.

“Ambacho tunakifanya kwa sasa ni kumsubiri mchezaji mwenyewe kwani anajua anachohitaji, kisha tutafanya naye mazungumzo ya kuboresha mkataba wake kwa kuwa bado ana mwaka mmoja, tunataka aendelee kula mema ya nchi,” alisema Kamwe.

SOMA NA HII  KISA UBINGWA...ALLY KAMWE ATAKA MASHABIKI YANGA WASIMSIKILIZE MANARA.....