Home Uncategorized EXCLUSIVE: STRAIKA RWANDA ASAINI YANGA MIAKA MIWILI

EXCLUSIVE: STRAIKA RWANDA ASAINI YANGA MIAKA MIWILI


Kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Rwanda, Issa Bigirimana amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea klabu ya Yanga akitokea klabu ya APR ya Rwanda.

Usajili huo umefanyika kutokana na pendekezo la Kocha Mwinyi Zahera ambaye amepewa majukumu yote hivi sasa ya kuchagua wachezaji.

Huyu anakuwa mchezaji wa pili wa Yanga baada ya kumalizana na Tshishimbi aliyeongeza pia miaka miwili.

Usajili umeendelea kushika kasi hivi sasa ikiwa ni baada ya ligi kumalizika juzi.

SOMA NA HII  ISHU YA KUANZA KIKOSI CHA KWANZA KWA NYOTA WA SIMBA IPO HIVI