Home Habari za michezo SIMBA IJAYO NI UTAMU MWANZO MWISHO…..DILI LA MIQUISSONE ‘UPDATE’ HII HAPA…

SIMBA IJAYO NI UTAMU MWANZO MWISHO…..DILI LA MIQUISSONE ‘UPDATE’ HII HAPA…

Tetesi za usajili Simba

IMEBAINIKA kuwa, uongozi wa Simba umelipitisha jina la Luis Jose Miquissone kuwa usajili wao mkubwa msimu ujao kupitia dirisha kubwa ambalo litafunguliwa hivi karibuni.

Luis Miquissone anakumbukwa kwa mengi makubwa aliyoyafanya pindi alipokuwa mitaa ya Msimbazi kuanzia Januari 2020 hadi Agosti 2021 alipotimkia Al Ahly ambapo ameshindwa kufanya vizuri.

Kwa sasa Miquissone hayupo ndani ya Al Ahly baada ya klabu hiyo kumtoa kwenye mipango yao na kusema wapo tayari kumuuza.

Chanzo cha ndani kutoka Simba, kimebainisha Simba kuwa na mpango wa kumrudisha Luis Miquissone ndani ya timu hiyo na kuwa usajili wao mkubwa wakiamini wanaweza kumpata kutokana mahusiano mazuri baina ya Simba na Al Ahly.

“Simba wana mahusiano mazuri na Al Ahly, hivyo wanachotaka kukifanya ni kuhakikisha wanakamilisha usajili wa kumrudisha Luis Miquissone ndani ya Simba.

“Ni usajili ambao kwao wamepanga kuwa usajili mkubwa kupitia dirisha hili kutokana na uwezo wake ambao amewahi kuuonesha ndani ya Simba kuwashawishi mashabiki wengi ambao wanatamani arudi, Simba wapo katika mazungumzo mazuri ya kumrudisha Miquissone na huenda dili likatimia,” kilisema chanzo hicho.

SOMA NA HII  WAKATI WENZAO WAKIWA KWENYE TIZI KALI...UONGOZI YANGA WAFUNGUKA A-Z WALIPO BANGALA NA MORRISON..