Home Habari za michezo TETESI…SIMBA SC WAPANIA KUMNG’OA JOB YANGA….MKATABA WATAKAO UMPA HUU HAPA…

TETESI…SIMBA SC WAPANIA KUMNG’OA JOB YANGA….MKATABA WATAKAO UMPA HUU HAPA…

Habari za Simba SC

Nyota wa kimataifa wa Tanzania, Dickson Job anaelekea kwenye miezi ya mwisho ya mkataba wake Jangwani na tayari timu kadhaa zinahitaji huduma yake.

Simba SC, wao wanahitaji huduma ya nyota huyo na tayari jitihada za haraka zimefanyika ili kuinasa saini yake, wameshaweka ofa nono mezani pamoja na mshahara ambao ni mara tatu ya anachopata hivi sasa, taarifa za uhakika ni kuwa Simba SC wanasubiri β€˜account number’ yake tu.

Taarifa kutoka kwa mtu wa karibu na nyota huyo, zinadai kuwa Simba SC wako tayari kumpa mshahara wa milioni 10 kwa mwezi, pamoja na kumpa ada ya usajili ya Milioni 300.

Ofa hiyo ni kubwa zaidi ya Yanga SC, ambapo wao inasemekana wanataka kumpa ofa ya mshahara wa Milioni 7 pamoja na ada ya usajili ya Milioni 200.

Kwa upande wao Azam wameulizia upatikanaji wake na walichoambiwa ni kuwa kama wapo tayari kwa ajili ya mazungumzo basi wakutane ili watimize matakwa yake yote ya kimkataba, hili ni juu yake.

Huku hayo yakijiri, Yanga wamemwita na kuzungumza naye na wametaja dau lao (signing fee) na mshahara, ingawa inasemekana hajasaini karatasi yoyote ya Yanga mpaka hivi sasa.

Dickson amekuwa beki tegemeo ndani ya kikosi cha Yanga SC, ambapo amefanikiwa kushinda mataji mawili makubwa ikiwemo Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho, huku wakiingia hatua ya makundi kombe la shirikisho Afrika.

Kwa msimu huu Dickson amekuwa na uhakika wa kuanza kwenye kikosi cha Nabi, tofauti na wenzake, ambapo mara nyingi huwa akichezeshwa na Mwamnyeto au Bangala.

Dickson Job alisajiliwa na Yanga SC msimu miwili iliyopita akitokea Mtibwa Sugara ambapo alianzia soka lake huko.

SOMA NA HII  KAZE AKIRI PRESHA ILIKUWA KUBWA KWAKE