Home Habari za michezo PAMOJA NA KUWA BOSI WA MICHEZO NCHINI…ALLY MAYAI AMPA UFALME MOSES PHIRI…

PAMOJA NA KUWA BOSI WA MICHEZO NCHINI…ALLY MAYAI AMPA UFALME MOSES PHIRI…

ALIYEKUWA nahodha wa Klabu ya Yanga na Timu Taifa (Taifa Stars), ambaye kwa sasa ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini, Ally Mayayi Tembele, amempa alama zote mshambuliaji wa Simba, Moses Phiri kuwa ndiye nyota wa mchezo wa watani wa jadi

Simba na Yanga juzi zilitoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, shukran kwa Augustine Okrah na Stephanie Aziz Ki waliozifungia timu zao.

Mayayi, alisema licha ya mshambuliaji huyo wa Simba kutofumania nyavu, lakini mikimbio yake ilionekana kuwa na madhara zaidi kwa wapinzani wao.

“Kwangu mimi nyota wa mchezo alikuwa Moses Phiri, licha ya kutofunga, kwani ukimwangalia alikuwa ni mchezaji ambaye alikuwa ana madhara sana upande wa Yanga.

“Mikimbio yake ilikuwa ikiwasumbua wapinzani, Aziz Ki amefanikiwa kufunga bao bora lakini hakuwa na madhara kama ilivyokuwa kwa Phiri, ambaye alikuwa na umiliki wa mpira kwenye safu ya ulinzi ya Yanga,” alisema Mayai.

Akitathmini mchezo mzima wa juzi, Mayayi alisema: “Ukiangalia timu zote zilicheza 50 kwa 50, makocha walijificha sana kwenye tahadhari ya ulinzi kabla ya kwenda kushambulia, timu zote zilipoteza nafasi ya kufunga.

“Tahadhari ya ulinzi ilikuwa kubwa, kipindi cha pili, Yanga walitengeneza nafasi lakini hawakuwa na utulivu, hii ni kutokana na presha kuwa kubwa, Yanga ilikuwa na walinzi sita na Simba vilevile, hivyo utahadhari wao wa kujilinda ndio usababisha sare.

“Kwa upande wa makocha, Mgunda (Juma) na Nabi (Nasreddine), ni makocha wanaotumia falsafa zinazofanana kwa kutaka timu zao zichezee mpira, wana wachezaji wazuri wanaoweza kuwasaidia,” alisema.

SOMA NA HII  KISA SIMBA NA MASHINDANO YA SUPER LEAGUE...UWANJA WA MKAPA KUPIGWA MSASA UPYAA...