Home Uncategorized YANGA: HATUNA HOFU, TUPO TAYARI KUICHAPA SIMBA

YANGA: HATUNA HOFU, TUPO TAYARI KUICHAPA SIMBA


UONGOZI wa Yanga, umesema kuwa upo tayari kwa mchezo wao wa kesho, Machi 8 dhidi ya Simba utakaochezwa Uwanja wa Taifa kutokana na mipango waliyojiwekea kwenda sawa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Makamu Mwenyeiti wa Yanga, Fredric Mwakalebela amesema kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu ila wamejipanga kuona namna gani wataibuka na ushindi.

“Mchezo utakuwa mgumu ila tumejipanga kisawasawa kuona namna gani tunaibuka na ushindi, kikubwa ninapenda kuwaambia mashabiki wajitokeze kwa wingi Uwanja wa Taifa kushuhudia burudani itakavyokuwa.

“Hakuna haja ya kuhofia kwani kila mmoja anatambua umuhimu wa mechi ya kesho na kila mchezaji amepewa majukumu yake,” amesema.

Yanga ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo imejikusanyia pointi 47 baada ya kucheza mechi 24 huku Simba ikiwa nafasi ya kwanza imecheza mechi 26 na ina pointi 68 kibindoni.

SOMA NA HII  MBELGIJI WA YANGA AACHIWA KAZI YA KUCHAGUA WACHEZAJI ANAOWATAKA