Home Uncategorized MBELGIJI WA YANGA AACHIWA KAZI YA KUCHAGUA WACHEZAJI ANAOWATAKA

MBELGIJI WA YANGA AACHIWA KAZI YA KUCHAGUA WACHEZAJI ANAOWATAKA


UONGOZI wa Yanga umempa makali Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Luc Eymael kufanya uchaguzi wa wachezaji ambao anaona watafaa kuendelea kubaki ndani ya kikosi hicho.

Eymael, raia wa Ubelgji amepewa jukumu hilo kwa kuwa amekuwa akifanya kazi kwa ukaribu na wachezaji hao na Kamati ya Usajili ya Yanga haina mpango wa kumuingilia kwenye majukumu yake.

Habari zinaeleza kuwa kuna wachezaji saba ambao wanamaliza mikataba yao ndani ya klabu hiyo ya Yanga.

“Kuna wachezaji saba ambao mikataba yao inaisha hivi karibuni huku wengine wakitazamwa kwa ukaribu maendeleo yao kabla ya kocha kuamua abaki na nani ndani ya kikosi,” ilieleza taarifa hiyo.

Mongoni mwa wachezaji ambao inaelezwa kuwa mikataba yao inakaribia kuisha ni pamoja na Said Juma Makapu, Deus Kaseke, Mrisho Ngassa, Juma Abdul, Kelvin Yondani, Jaffary Mohamed, Vincent Andrew.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga. Fredirick Mwakalebela amesema kuwa mpango mkubwa kwenye suala la usajili ni kuongeza wachezaji makini ambao watakuwa na mchango mkubwa ndani ya Yanga.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO