Home Uncategorized CIOABA NA MINZIRO KWENYE MTIHANI MWINGINE LEO TAIFA

CIOABA NA MINZIRO KWENYE MTIHANI MWINGINE LEO TAIFA

 AZAM  FC, iliyo chini ya Arstica Ciaoba, leo ina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Alliance kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Taifa.

Machi 7 Alliance watakuwa wageni wa Azam FC wakiwa na kumbukukumbu ya kuchapwa mabao 2-0 mchezo wao wa mwisho waliocheza Uwanja wa Taifa msimu huu mbele ya Yanga huku wakiwa na kichapo kingine cha bao 1-0 walichokipokea kutoka kwa Ruvu Shooting, Uwanja wa Mabatini.

Kwa upande wa Azam FC itashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wake uliopita mbele ya Simba kwa kufungwa mabao 3-2 licha ya waoa kuanza kufunga dakika ya nne kupitia kwa Nevere Tegere.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Nyamagana, Alliance iliyo chini ya Kocha Mkuu Felix Minziro ilikubali kichapo cha mabao 5-0 .

Azam FC kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ipo nafasi ya pili ikiwa imejikusanyia pointi 68 na Alliance ipo nafasi ya 13 ikiwa imecheza mechi 26 ina pointi 29.

SOMA NA HII  YANGA YATOA TAMKO KUHUSU DANTE, JUMA ABUDL