Home Simba SC GOMES : TUKIAMUA HAKUNA WAKUTUZUIA

GOMES : TUKIAMUA HAKUNA WAKUTUZUIA


BAADA ya kufanikiwa kupenya mbele ya Azam kwa kuwafumua bao 1-0 kwenye mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC), juzi kwenye Uwanja wa Majimaji, mjini Songea, Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes ametamba na kikosi bora ambacho hakuna timu ya kuizuia tena. 

Gomes aliyasema hayo mara baada ya kumalizika kwa pambano hilo, lililojaa ufundi, nguvu na ubabe mwingine kabla ya bao la jioni la Luis Miquissone na Mfaransa huyo alifunguka anakiamini kikosi chake kwani kina morali na mizuka ya kutafuta ushindi kila wakati jambo ambalo hakuna timu yeyote Tanzania inaweza kuwazuia kupata ushindi wakiamua.

“Nakiamini kikosi changu, nina wachezaji wenye viwango na ubora mkubwa, hilo wamelithibitisha tangu nimeanza kazi na linaongezeka kila siku hivyo tukiamua tunaweza kuishinda tumu yeyote, mahali popote,” alisema Gomes na kuongeza;

“Azam walikuwa bora, walizuia vizuri na kusoma mbinu zetu katika kipindi cha kwanza lakini hilo halikutuzuia sisi kupata ushindi kwani nilivyoona wanazuia mbinu ya kwanza ikabidi nifanye mabadiliko kwa kuwaingiza Kagere na Morrison ambao wameenda kuongeza presha mbele na mwisho wa siku kushinda mechi hii.”

Pia kocha huyo alizungumzia mechi za ligi zilizobaki ikiwamo ya fainali ya ASFC ambapo alisema wanahitaji kushinda kila mechi zote zilizo mbele yao ili kumaliza msimu wakiwa mabingwa zaidi.

“Ili uwe bingwa lazima ushinde, natamani sana tushinde mechi zote zilizobaki ili tuwe mabingwa, ni jambo ambalo litawezekana endapo wachezaji wataendelea kujituma kwa ajili ya timu, nawashukuru mashabiki wote wa timu hii kwani wanajitoa kuisapoti katika nyakati zote inapokuwa ikicheza,” alisema Gomes kuongeza;

“Kuweza kupambana hadi kutinga fainali inaonesha namna gani tunalitaka kombe hilo, sio sahihi kuuzungumzia mchezo huo kwa sasa lakini najua tutacheza na Yanga, moja ya timu nzuri ila tutahakikisha tumeshinda na kutimiza malengo yetu.” Baada ya kumalizana na Azam, sasa Simba inajiandaa na mechi ya kiporo ya Ligi Kuu Bara dhidi ya watani zao Yanga.

SOMA NA HII  UKWELI MCHUNGU...KWA YANGA HII YA LEO..SIMBA WAPEWE MAUA YAKE TU MAPEMA...