Home Habari za michezo SKUDU NA SAKATA LA JEZI YA FEI TOTO YANGA

SKUDU NA SAKATA LA JEZI YA FEI TOTO YANGA

Habari za Yanga

Nyota mpya wa Yanga,Mahlatse Makudubela’Skudu’ amesema hakuchagua kutumia jezi namba sita bali alichaguliwa.

Skudu amezungumza hayo leo muda mfupi kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa hakuwahi kuivaa jezi namba sita kwenye timu yoyote.

Aidha alisema haikuwa rahisi kuchagua namba sita ambayo ilikuwa na kitendawili na presha kubwa.

“ Sikuichagua namba sita ila klabu ndio imenichagulia kabla ya Yanga sijawahi kuvaa jezi namba hiyo nilikiwa navaa namba 11 waliniambia wangependa kunipa jezi namba sita na nilisema ni heshima kwasababu niliona presha ya jezi hiyo na kila mtu anakuwa kulingana na presha” amesema Skudu

Skudu alitambulishwa Julai 18 na kupewa jezi namba 6 ambayo iliachwa wazi na kiungo wa zamani wa Yanga Feisal Salum ‘Fei Toto’ aliyeuzwa Azam FC.

Skudu amewahi kucheza Timu mbalimbali zikiwemo Mamelod Sundowns, Orlando Pirates, Highland Park na Chippa United zote za Afrika Kusini.

SOMA NA HII  HII HAPA ORODHA YA WASHINDI WOTE WA TUZO ZA CAF JANA USIKU...SENEGAL WATAWALA MWANZO MWISHO....