Home Uncategorized YANGA YAMTAJA ALIYEKABIDHIWA MIKOBA YA ZLATKO

YANGA YAMTAJA ALIYEKABIDHIWA MIKOBA YA ZLATKO

 


INJINIA Hersi Said, Mjumbe wa Kamati ya Usajili ndani ya Klabu ya Yanga na Mkurugenzi wa Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa klabu hiyo amesema kuwa benchi la ufundi linabaki chini ya Juma Mwambusi ambaye alikuwa ni kocha msaidizi wa klabu hiyo.


Mwambusi alikuwa akifanya kazi chini ya Kocha Mkuu, Zlatko Krimpotic ambaye alifungashiwa virago vyake ndani ya Yanga Oktoba 3 muda mfupi baada ya kutoka kukiongoza kikosi chake kushinda mabao 3-0 mbele ya Coastal Union.

Hersi amesema:”Kwenye benchi la ufundi ameondolewa Zlatko peke yake, hivyo kwa sasa timu itakuwa chini ya Juma Mwambusi pamoja na wale wengine aliokuwa akifanya nao kazi.

“Kikubwa kwa sasa tunaangalia namna gani tunaweza kumpata mrithi wake ila hakuna kitakachoharibika kwani mipango inakwenda vizuri mashabiki na wadau wasiwe na mashaka taarifa watazipata muda sio mrefu.”

Zlatko amekiongoza kikosi kwenye mechi tano za ligi ambapo alilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Tanzania Prisons na alishinda mechi nne akifikisha jumla ya pointi 13 kibindoni.

Kwenye mechi zake zote ambazo alikuwa benchi timu yake haikupoteza mchezo.

SOMA NA HII  TAMBWE:YANGA WANAPASWA KULIPA FEDHA ZOTE,WASIPOFANYA HIVYO WATAJUANA NA FIFA