Home Uncategorized YANGA: TUNALIPA KISASI KWA TOWNSHIP ROLLERS AGOST 10

YANGA: TUNALIPA KISASI KWA TOWNSHIP ROLLERS AGOST 10


DISMAS Ten, Kaimu Katibu wa Yanga amesema kuwa kwa sasa wamejipanga kufika mbali kwenye michuano ya kimataifa hivyo wataanza kazi na Township Rollers Agosti 10.

Yanga itamenyana na Township Rollers uwanja wa Taifa, mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa utakuwa Jumamosi 

Akizungumza na Saleh Jembe, Ten amesema kuwa wanawatambua vema wapinzani wao hivyo wana imani ya kupata matokeo chanya kwenye mchezo wao wa kwanza.

“Mchezo utachezwa Agosti 10 uwanja wa Taifa hivyo nawaomba mashabiki wa Yanga watupe sapoti, mara hii tunataka kufika mbali zaidi ya tulipofika zamani na wajitokeze kwa wingi.

“Rollers ni timu nzuri na tunawajua, mara ya mwisho walitutoa sisi hivyo sasa tunataka tuwatoe sisi ili tusonge mbele zaidi ya pale tulipoishia,” amesema.

SOMA NA HII  DAR ES SALAAM CORRIDOR GROUP KUMUONA MO SALAH LIVE ANFIELD