Home Uncategorized STRAIKA HATARI ORLANDO PIRATES KUTUA SIMBA, AAGA RASMI

STRAIKA HATARI ORLANDO PIRATES KUTUA SIMBA, AAGA RASMI


Simba ipo kwenye mipango ya kukamilisha taratibu za kumsajili mshambuliaji mzambia wa Orlando Pirates ya nchini afrika kusini, Justin Shonga.

Timu hiyo imepanga kufanya usajili bab kubwa katika kukiimarisha kikosi chao kinachojiandaa na Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu Bara. Simba hadi sasa imewasajili wachezaji wawili ambao ni Beno Kakolanya aliyekuwa Yanga na Kennedy Juma wa Singida United.

Taarifa ambazo Championi Jumatano imezipata kutoka kwenye mtandao mmoja maarufu wa Afrika Kusini, mshambuliaji huyo ana ofa mbili mezani kutoka Eibar ya Hispania na Simba ambayo imeonyesha nia kubwa ya kumsajili.

Mtandao huo unasema kuwa, Shonga tayari amewaaga viongozi na mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia msimu ujao hatakuwa na Pirates, badala yake atajiunga na timu mojawapo kati ya hizo.

Wakati Shonga akiaga, mashabiki wa Pirates walimshauri kwenda Eibar, huku wale wa Simba wakimkaribisha kikosini kwao.

Bodi ya Utendaji ya Simba chini ya bilionea, Mohammed Dewji, imeahidi kufanya usajili bora na wa kishindo kwa kusajili mshambuliaji mwenye uwezo zaidi ya Meddie Kagere na John Bocco.

“Tumedhamiria kufika mbali kwenye michuano ya kimataifa, ikiwezekana kuchukua ubingwa, hivyo tumepanga kusajili mchezaji yeyote tutakayemhitaji ndani ya Afrika,” alisema Mo Dewji.

SOMA NA HII  CORONA YAZIDI KUWA TISHIO KWA WAAFUNZI WATANZANIA, SERIKALI NCHINI YATOA TAMKO