Home Habari za michezo KISA KUSIMAMISHWA SIMBA….KAPAMA AVUNJA UKIMYA….AFUNGUA A-Z KINACHOENDELEA…

KISA KUSIMAMISHWA SIMBA….KAPAMA AVUNJA UKIMYA….AFUNGUA A-Z KINACHOENDELEA…

Habari za Simba

UONGOZI wa klabu umewasimamisha wachezaji wake wawili viungo, Clautos Chama na Nassor Kapama kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu.

Taarifa kutoka idara ya Habari na Mawasiliano Simba inayosimamiwa na Ahmed Ally imesema hatua hiyo ni kufuatia vitendo vya utovu wa nidhamu kwa wachezaji hao watapelekwa katika Kamato ya nidhamu iliyopo chini ya Kamanda wa Polisi wa zamani wa Mkoa wa Dar es Salaam, Seleman Kova.

Ilisema nyota hawa watapelekwa kwenye kamati hiyo kwa ajili ya kuchukuliwa hatua zaidi za kimidhamu.

“Simba imekuwa na utaratibu wa kuwapeleka kamati ya nidhamu wachezaji ili nao wao wapewe nafasi ya kusikilizwa kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa dhidi yao.

Uongozi unapenda kuwakumbusha watumishi wake kuzingatia misingi ya maadili na nidhamu kwani klabu haitasita kumchukulia hatua yeyote atakayethibitika kwenda kinyume na utaratibu huo,” ilisema taarifa hiyo.

Alipotafutwa Kapama alisema taarifa hizo ameziona na ataenda katika kamati hiyo kusikiliza mashtaka yake.

“Kusema kweli sielewi, nimeona taarifa tu hivyo nitaenda kwenye kamati kusikiliza,” alisema nyota huyo.

SOMA NA HII  SAA KADHAA KABLA YA KUSHUKA DIMBANI LEO....YANGA WAPEWA 'USHINDI WA MEZANI' DHIDI YA WASUDANI...ISHU NZIMA IKO HIVI...